Maelekezo ya Misa ya huruma ya Mungu tarehe 8 Aprili 2018 yametolewa!

Image result for pope francisKwa mujibu wa Ofisi ya Maandhimisho ya Liturujia za Papa inatoa taarifa kuwa:  Tarehe 8 Aprili 2018 Jumapili ya II ya Pasaka au ya Huruma ya Mungu, saa 4.30 Asuhuhi masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. kwa maana hiyo wanawakaribisha kwa wote watakao adhimisha na Papa,wakiwa  Makardinali, Mapatriaki, Maaskofu wakuu na maaskofu wengine, wakutane saa 3.45 katika Kanisa dogo la Mtakatifu Sebastian ndani ya Kanisa Kuu wakiwa na nguo za maadhimisho.

Pia Wamisionari wa Huruma ya Mungu na wote walio na vibali vilivyotolewa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Uinjilishaji mpya wataukana saa 3.00  asubuhi katika sehemu ya Mkono wa Constatino. Aidha kwa Mapadre ambao wamepata vibali kutoka katika Ofisi ya maadhimisho ya Liturujia za Papa wanatakiwa pia kukutana saa 3.00 katika Kanisa dogo la Kutolewa Bwana Hekaluni, ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Imetolewa na mwandaaji wa Maadhimisho ya Liturujia za Papa  Monsinyo Guido Marini.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

No comments